Now Reading
Mapinduzi Ya Kusimama Wima Ama Kwanini Wasee Hu-Walk –Wima

Mapinduzi Ya Kusimama Wima Ama Kwanini Wasee Hu-Walk –Wima

The Upright Revolution 4


Sheng

Mwas Mahugu

Hapo tene jo! Wasee walikua wanawalk na miguu na mikono, ka venye maanimals zile huwalk na miguu nne. Mraia ilikua ina toka nduki kushinda kaka sungura, chui ama kifaru. Milegi na mikono zilikuwa zimekaribiana kushinda organs zingine; majoints zilikuwa in-sync; mashoulder na hips; elbow na magoti; kisigino na ngumi, milegi na guoko, kila ikiisha na vidole na mafingers tano, na kucha kwa mikono na miguu. Mikono na milegi na maarrangement kutoka kwa toes na mikono, kutoka ile kidole bwaku hadi ile smalls walikuwa close. Hizo siku tunaskia hii story walikuwa hadi wanaitana ma-cuuzo wa first.

Wali kuwa wanapeana back up kupeleka mwili place any ilikua inataka kuishia; soko, duka, ma-roundi za ku-climb miti na pia milima, place yeyote mwili ili kuwa inataka kwenda. Hata ndani ya maji, walichapa works pamoja ndio body i-float, i-swim ama kuingia kiindie – story na duufo. Pia miguu na mikono ilikuwa inaitisha back up ya organs ziko sekta ingine ya mwili, tuseme sauti kutoka kwa mdomo, kusikia ya kunusa ya mapua-na kucheki ya macho.

Ma-waves za coordination na hizi rhythm zilikuwa zina bamba part zingine za body; walikuwa wanaleta shangwe kwa kuspice ugenius kwa macuzo. –wivu Kalikuwa kana wa- blind juu miguu a mikono ilisha chukua places. So beef ika develop wakaanza –kupangia njama hizo part mbili.

Kaka Ulimi akachora plan akisaidiwa – na brain na kuiweka kwa meza mara moja. Ulimi baadaye akapigwa na mshangao; juu ya power miguu na mikono, nani alikuwa ngori kati ya hawa macuzo wawili limbs, wale hawakuwa hata wanaelewa msee mwingine alikuwa ana-do nini, roundi this waka-borrow sauti kutoka kwa Mdomo, na wakadai title ya kuwa-wa maana kuliko hizo parts zingine. Hii story ilianza ku-change eti nani ana swagg; Mikono ilidai title ya kuwa na fingers za nguvu, na kuchongoa vidole za miguu vile zilikua nono na short. Kuskskia hivo, Vidole za miguu zika counter hiyo claim, na kwambia Fingers vile zilikuwa konda,! ma-cuzo walikua wana kufa ubao! Hii story ili endelea siku kadhaatime zingine mpaka ika leta ngori mambo na kufanya kazi pamoja vile inafaa, story yote ilifika evel ya nani ako na power; manze ikabaki wame ita organs zingine kesi iwekwe mezani.

Ilikuwa Ulimi aliye suggest ka compee, bonge la idea, kila msee aka agree “Hebu acha? Wengine waka suggest mechi ya miereka, kuangushana wengine waka dai ku-fight na sword, juggling, kutoana mbio, kucheza game ka chess ama checkers lakini kila game ika kaangumu kiasi pia ilikuwa inakaa un fair kwa part zingine. Ulimi kama kawa tena after kuitisha back up ki-branwise kutoka akili `akarahisisha mambo, kila part ya body waka- agree ilete game yake in turns, so kila part, mikono na miguu zika agree.

Place ya mechi ilikuwa ni space katikati ya msituyenye ilikua open, karibu na River. Viungo zote zilikua rada ndio danger isitokee ipate mwili na surprise. Juu unashikanisha viungo zote zilikuwa zinapimana nguvu. Macho zilitupa darubini far sana kucheki ka kuna ngori kona zote; Masikio nazo zilikuwa rada kuziskiza sauti kutoka kona zote, kaka Pua nayee akanusa na kuclear ndio aweze kucheki ngori yenye maybe ilipita bila macho na maskio kuona na kusikia, nayee Ulimi alikuwa ready kushout na kuscream ngori ikitokea.

Upepo ilifikisha news kona zote nne za hii msitu, maji na hewa. Animal zina miguu nne zilikua za first kufika, zile biggi biggi zikiwa zimebeba matawi ya green kushow zilikuja kwa amani, ilikua umati ya power na kufurahisha macho. Kaka Chui, kaka Cheetah, kaka Simba, kaka Rhino, kaka Fisi, kaka Ndovu, kaka Twiga , kaka Ngamia, ngo’mbe zina pembe bwaku na nyati zilio na pembe fupi, Bongo, Swara, kaka Sunguch, huko na Panya na pia raia ya kuishi chini ya maji ka Hippo, fish, mamba, waka toa mavichwa kutoka ka maji ndio wapate view poa; part zingine zikiwa bado kwa maji ya rivay.

Zile raiya zina miguu mbekse ka ostrich, guinea fowl, na tausi zikachapa ma-wings kwa hewa juu ya kubambika, ndege na ma-dush zikakuwa kwa mix juu ya miti, macricket kama kawa zili imba all the time, bui bui, worm, centipede, millipede zili jivutavuta toka kwa miti na pia chini ya ground. Kinyonga aliingia mdogo mdogo, bila hurry, Lizard naye alikua teke teke na alikua ana move sides zote bila kutulia. Nyani, Tumbili, Gorilla, zili rukaruka kutoka kwa branch. Hata miti na bush, zilimove gently side to side, zikabow down alafu zikatulia mara kwa mara.

Mdomo alifungua hii compee Na song:

Si hufanya hii kujibamba
Si hufanya hii kujibamba
Si hufanya hii kujibamba
Juu sisi wote tunakoka ka source moja nature

Mikono na miguu ika show kila msee wata accept results kwa unyenyekevu, bila kuleta noma na pang’ang’a, vitisho, kuzusha, kustrike ama kujivutavuta.

Mikono ili peana challenge – ilutupa kambao hapo chini kwa kiwanja, miguu nayo kushoto kulia hapa kule ikapiga kombi, mguu ilikuwa uchukue kale ka mbao kutoka chini na kukarusha, miguu ilisikizana ama kuulizana back up ya move wakati wowote wa compe, na kutuma kidole moja ama zote at a go, ndio mission itimike vifreshi.

Wali jaribu kuturn over na kusukuma, waka jaribu combination zote. Lakini hawakutoboa vipoa; na mambo na kuisongesha kiasi, best way wangetoboa ni kupiga teke inches kadhaa. Kuona hivi, vidole wakabonga na Mdomo apititshe sauti, so akacheka na kucheka vibaya sana. Mikono machallenger, waka panga foleni ka jeshi, lakini nikaa beauty contest ya ma-models, waki-showcase finger zao slim, so combinations kadhaa zikachukua kale kambao kwa floor .Wakaitupa farthest sana kwa Forest, hiyo throw iliacha maspectator hoi; wakafurahi na mshangao sana. Wali show Raia skills zingine; waka chukua tupiece twa mchanga kutoka kwa bilauri ilikua na Mchele. Walishona na wakamake pulley za kusongesha mbao mzito. Waka-make mikuki na kuzithrow far, moves ziliacha vidole za miguu na daydreams, miguu zilikula meditation zikishangaa na game ya fingers za mkono – flexibility ya hawa macuzo ilikuwa ngori.

Mikono mashabiki walipiga makofi ya ngurumo wakipigwa back up na mikono. Miguu hawakubambika na hiyo story; walijam sana lakini jo hawakuwa ready kuitikia hii story, hata kaa walikaa hapo wakikaa kiradar – vidole za miguu zikichora mamap kwa mchanga, miguu ilikuwa inachora vile ingevuka na hii title.

Mara ya mwisho, time ilifika Miguu na Toes kuissue a challenge, yao walidai ilikuwa simple sana, walidai Mikono ichukue body kutoka side moja ya circle
mpaka hiyo side ingine. “Hii challenge ilikuwa ya kifala,” finger zilidai hii ilikuwa sight jo. Kila kitu ya body ilikua upside down, mikono zilikua zimeguza chini, macho zilikua karibu na ground,na hazikua zinaona poa kwa hii angle; vumbi ikaingia mapua jo!na pua ikapiga chafya; miguu na toes zilifloat kwa hewa: nyayo juu, mafans walishout, na kudance huku waki-sing.

Nyayo Nyayo juu
Hakuna matata
Fuata Nyayo
Hakuna matata
Turukeni angani.

Lakini attention ilikuwa fixed on hands na miguu. Maparts za body zile zilikuwa zinashow maskill hapo awali, this time hata haikumake any move. Steps kiasi; mikono Ililia juu ya pain, arms zikastagger, kushakeshake, na ikaachilia body ikafall.

Walikula cover kiasi na kupumzika na wakamake attempt ingine. Roundii hii walitry kuspread fingers vipoa ndio zishikilie chini mchangani, lakini thumbs tu ndio zilitoboa kustretch .Walijaribu kupiga cartwheel but hiyo mchezo ili kataliwa juu ilibidi miguu zikuje on board, so ilikuwa turn ya toes kucheka mbaya. Wali-borrow sauti heavy za throat kutoka mdomoni ili ku balance contrast ya kicheko funny vidole zilikua zime tumia. Kusikia hii dharau mikono zika jam na zika jaribu kubeba mwili lakini wapi! Hawa kutoboa hata step moja juu ya uchovu na kuchoka kwa hands na vidole zikaacha hii mambo. Miguu ili bambika kushow nguvu za kutoka teke, wali mark time, kuenda na kurudi, kukimbia, waka make high jump kadhaa pia malong jump bila kuachilia body ianguke. Mashabiki wote wa feet wakastamp chini kama masoldiers na kuitikia kwa umoja. Mikono ziliamsha hands juu kuprotest hii move bila kusahau hao wenyewe ndio walianza hii game.

Lakini wasee wote, hata mafans, walinotice kitu strange na mikono; vidole za gumba zilikuwa zimestretch out wakati hands zilikuwa zina jaribu kubeba mwili, na zilikuwa zimejitenga na vidole zingine. Marival organs zilikuwa karibu kurudia kicheko lakini zikanotice kitu ingine tofauti; hata ka kidole cha gumba kilikuwa far ikija ni kushikilia kitu, story ni eti walikuwa na power ya kushikilia na kukumbatia. Hii ni nini jo? Yaani hii blunder ya separation ilikuwa yenyewe ndio key kushikilia vitu na power!

So manze debate ya kuamua nani winner kati ya organs za mwili iligo siku tano jo, hii number ya fingers na toes kwa kila limb. Walijaribu sana but still hawa ku-manage kupata winner nani ndio kusema; kila limb ilikuwa poa na kazi yake; hakuna angetoboa bila mwingine. Walianza kuchambua hii maneno na kuspeculate. “Kwanza mwili ilikuwa ni nini?” waliulizana na kumbe waka discover body ilikuwa hao wote pamoja; walikuwa wameshika ka kila part iki wakilisha ingine. Kila organ ilikuwa ichape works poa ndio hiyo part ingine ifanye works poa.

Lakini jo ndio kuavoid mashindano in future, na kuavoid hizi organ kugongana na kupatana njiani, wote walidecide kitu moja, kutoka siku hiyo mwili iianze kutembea wima, miguu zikiwa chini kwa ground na mikono hewani. Mwili ilibambika na hii decision, lakini mwili ilimake point – itakuwa inaruhusu watoto watembee na miguu nne ndio wasisahau walipotoka; history muhimu. Wakagawana works na roles: miguu ingecarry body kuenda place yeyote but wakati ilifika mwisho wa safari, alafu mikono zinge take over na kufanya works ya kushikilia vitu.

Hata kaa miguu ndio zilikuwa zinafanya kazi mob na kazi ngumu ya kubeba, mikono nayo ilichangamka na kutumia maskills mwenda kuchapa works na kumake sure food ilifika mdomoni, nayo mdomo ama meno ilichew nakuituma kwa throat nayo ikiiteremka hadi kwa tumbo. Tumbo nayo ilisqueeze utamu wote na kurusha kwa canal za system na hapa utamu na uzuri ungegawanywa kwa kona zote za mwili. Tumbo ingerusha waste kwa sewage system, nayo body ingechangamka na kutafuta kabush nakudeposit viwanjani ama kuzika chini ya mchanga ili ipate fertilizer. Nazo plants zingegrow na kuzaa mafruits, mikono kama kawa zingepick hizi fruits na kuziweka mdomoni. Aha! Hii ndio ilikuwa circle ya life.

Hata magames na kujibamba ziligawanyishwa, kuimba, kucheka na kubonga ziliachiwa mdomo, kutoka mbio na kucheza fuuta zikaachiwa miguu, games kama bakey na baseball zikaachiwa mikono, lakini wakaagree miguu ndio ilikuwa ina run, mambo na mbio miguu ilikuwa solo – hii sekta-kiwanja ilikuwa yao. Hii kitu clear ya kugawana works ilifanya body kuwa machine ya nguvu, machine ilikuwa inashinda hata wanyama wabiggi yaani what ingemanage kufanya in quality na quantity.

Baadaye wakarealize hii mpangilio permanent walikuwa wamepanga in future inaezaleta beef na ugomvi. Kichwa ikiwa hapo juu ingefeel ilikuwa poa kushinda feets zilitouch chini, ama kichwa ndio master na wasee wote wako below ni maservant pekee. So walisisitiza mambo na power, kichwa na yeyote ako chini wote walikuwa equal. Kupiga line ya capital letters hapa, kila kiungo wali make sure kama kubambika na uchungu ingekuwa shared kwa parts zote za body. Mdomo ilipewa onyo kali anytime ikisema vitu zangu na zile, ilikuwa ina bonga kuhusu mwili yote na si kama sole owner.

Wakaimba:

Hakuna mtumishi
Kwa mwili yetu
There’s no servant
Hakuna mtumishi
We serve one another
Tunaserve-kuserviana
Tunaserve –tunaserve
Sisi kwa sisi
Tunaserve-kuserviana
Tunatumikiana
sisi
Tunatumikiana
Ulimi sauti yetu
Nibambe nikubambe
Tunajenga body ina afya
Nibambe nikubambe
Tunajenga body ina afya
Urembo ni umoja

Pamoja tuchapa works
Kwa body in afya
Pamoja tuna chapa works
Kwa body ina afya
Umoja ni power

Hii ikawa ndio anthem ya Mwili. Mwili husing hadi wa leo, na hii ndio tofauti ya msee na wanyama, ama wale walikataa mapinduzi yakuwalk wima.

Hata baada ya kucheki hio scenario, wanyama wakuwalk na miguu nne hawakukubali hii mapinduzi. Hii biz ya kuimba ilikuwa funny kivyake na ya kifala. Mdomo ilitengenezwa kukula na wala si kuimba. So wakaform chama cha kutunza maumbile na wakashikanisha tabia hazibadiliki.

Wakati binadamu wanasoma na kujua kutoka kwa network za viungo, wanafanya mambo poa na wako fine; lakini wakati wanaona mwili na kichwa wakifanya vita ama kama viungo za vita, kila part ikingurumia ingine, wana karibia macuzo wao wanyama walio kataa mapinduzi ya kusimama wima.

~
Edited by Monaja Monch Kimenchu
Read the English translation – The Upright Revolution: Or Why Humans Walk Upright by Ngugi wa Thiong’o


Mwangi Wa Mahugu pen name Mwas Mahugu is a writer and an afro -hip hop artist, a pioneer sheng writer published by kwani Trust in several editions, his literature is inspired by people and it revolves around love and hate, conformity and rebellion, innocence and experience. He is the coordinating Trustee East Africa rise Up Project; a music & development movement project running CO-OP projects in Tanzania, Uganda, Kenya, and Malawi. When not writing, he is recording music, coordinating music events and managing artists. He writes to discover and to tell stories, since he believes artist and writers are mirror of society. Mwas is a part of jalada Africa collective.

What's Your Reaction?
Excited
0
Happy
0
In Love
0
Not Sure
0
Silly
0
Scroll To Top