Now Reading
Jalada 09: Kiu (Kiswahili)

Jalada 09: Kiu (Kiswahili)

Figure #90 from the series
“Quickly but carefully cross to the other side.”
Photo collage 63.5×64.5cm 2020
Artist: Ibrahim A. Ahmed

Dunia imebadilika na tunashuhudia kuyeyuka kwake.

Tuko wadhaifu kutokana na kitisho kikubwa kinachoweza kumithilishwa na hadithi zisizoaminika.

Ni kama ruiya; ndoto ya kutisha na kutolesha jasho usingizini. Sinema ya kuogofya. Hakuna jambo lenye uhakika lakini sote tunaunganisha na matumaini na hofu.

Tunaamini kuwa maisha yatakuwa bora tena. Tutashinda hatimaye.


Lakini kuna shida kubwa katika hamu hiyo ya kurudi kwenye maisha ya awali au yale yanayokubalika kama ya kawaida huko nyumbani, kazini, maishani mwetu, kwenye sanaa yetu, au kama inavyokubaliwa na jamii pana.  Hii ni fursa ya kuchunguza namna tulivyokuwa tumebadilika kabla ya COVID-19 kutulazimisha kubadili zaidi maisha yetu. Ni fursa ya kutazama kwa kina athari za mabadiliko ya polepole ya kitamaduni, kijamii na kisiasa.


Soma tangazo hili kwa lugha tofauti: Kireno, Kiingereza au Kifaransa.


Ni kwa njia zipi tumebadilishwa kutokana na  kuongezeka na kupotea kwa lugha, mimea na wanyama wa porini ama uharibifu wa mbingu, bahari, na ardhi? Ni jinsi gani tumetenganishwa au kukaribiana kutokana na mabadiliko haya? Ni nini tulichokihuisha au kukiunda? Ni nini matokeo ya kufanya kila kitu chombo cha biashara? Ni nini matokeo ya juhudi za kuwafanya watu wafanane, ijapokuwa wako tofauti?

Lakini kuna mabadiliko yasiyokuwa mabaya.  Binadamu yuko bora zaidi bila utumwa na ukoloni uliokuwepo siku zilizopita. Ushindi wa kampeni kupigania haki za uraia  na ukombozi wa wanawake pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia umekuwa na manufaa makubwa. Mabadiliko katika itikadi za fasihi na sanaa yametupeleka mbele.  Je, ni mabadiliko yapi yalifaa kuachwa jana au milenia iliyopita? Je, tunakumbuka au kujua haya malimwengu ya zamani?

KIU pia ni Saudade: hamu ya upendo iliyosalia au ambayo haikutendeka. 

Saudade (Kiingereza: / ˌsaʊˈdɑːdə /, Kireno cha Ulaya: [sɐwˈðaðɨ], Kireno cha Brazil: [sawˈdadi] au [sawˈdadʒi], Galilaya: [sawˈðaðɪ]; saudades ya wingi) ni hali ya kutamani sana jambo fulani au mtu fulani unayempenda.

Tunaelewa vipi jambo lisilokuwa limetendeka? Jambo hilo linaweza kuwa tumelitunga au lisilokuwa na kweli au tulilolijengea kumbukumbu? Je, tumejipatanisha na ahadi zilizowekwa zamani? Tumejisamehe kwa kutokuwa watu au mataifa tuliyopaswa kuwa kufikia sasa? 

Mkusanyiko huu wa kazi za kibunifu kuhusu KIU  ni uchunguzi wa kumbukumbu; utamaduni na hali ya kisasa; kinachoonekana na kisichoonekana; urithi na upotovu; vilio na uvumbuzi;, kinachowezekana na kisichowezekana.

UWASILISHAJI

1. KIU Mtandaoni
Tunakaribisha majibu ya suala laKIU mtandaoni. Jibu linaweza kuwasilishwa kama shairi na hadithi fupi, pamoja (au kando ya) picha, video na michoro asili. Pia, picha za kisasa kama GIFs na meme. 

Tujulishe kuhusu kazi yako kwa njia ya Facebook, Instagram na Twitter kupitia ukurasa wetu wa Jalada Africa. Tumia #JaladaNostalgia ili kuhakikisha tumeiona.

Anza kutuma kazi yako kuanzia Juni 1, 2020.

2. Mkusanyiko wa KIU 
Tunaandaa mkusanyiko wa hadithi fupi, mashairi, insha, sanaa, filamu na mahojiano (yaliyochapishwa kama matini, sauti au filamu) juu ya mada ya KIU.

Uwasilishaji utapokelewa baina ya Juni 1, 2020 na Julai 31, 2020.

Miongozo

Hadithi
Kila mwandishi anaweza kuwasilisha sampuli tatu za hadithi au maelezo mafupi. Hadithi zinapaswa kuruwazwa kama ifuatavyo: nafasi 1.5, Pt 12pt.  Font Times New Roman.

Ushairi
Tafadhali tuma mashairi matatu tu yasiyozidi kurasa 10. Mashairi yote ya mwandishi mmoja yanapaswa kutumwa kwa kiambatisho kimoja, na kila shairi likiwa na alama wazi. Ushairi unapaswa kuruwazwa  kama ifuatavyo: nafasi 1.5 Pt 12pt Font Times New Roman.

Insha
Tunakaribisha insha juu ya mada ya KIU zisizozidi maneno 7,000. Insha zinapaswa kuruwazwa  kama ifuatavyo: nafasi 1.5,Pt 12 Font Times New Roman.

Mahojiano
Tunakaribisha mahojiano na mazungumzo ya aina ya uandishi wa habari, sanaa, au fasihi kwa kujibu swali la KIU. Matini yanapaswa kuambatana na faili yenye sauti au picha.

Picha/Sanaa
Wasanii wanapaswa kuwasilisha kazi zao kama JPEGS (uimara: 72-150dpi; ukubwa usiopungua: 1024 × 768; nafasi ya rangi: RGB). Kila kipande cha sanaa kinapaswa kujumuisha habari ifuatayo: jina la kazi; mwaka iliyoundwa (na ikiwa msanii anahisi ni muhimu, maandishi mafupi ya maandishi / maelezo).

Mwongozo huu pia utatumiwa na wale watakaowasilisha kupitia lugha ya michoro, kama vile mashairi ya michoro, mabango na aina zingine zote za matini na uchapaji wa kuonyesha.

Zingatia:

1. Uwasilishaji wote lazima upelekwe kwa Jalada ya Afrika kupitia barua pepe kwa: jaladaafrica@gmail.com.

2. Kila hadithi inapaswa kutumwa kama kiambatisho tofauti cha Neno la Microsoft, katika ruwaza ya .doc (usitume PDF). Bainisha jina la hadithi na majina ya mwandishi au mfasiri. 

3. Kila uwasilishaji lazima uwe na jina la hadithi na hesabu ya maneno.

4. Itakapohitajika, tuma hadithi asili pamoja na tafsiri yake.

5. Uwasilishaji wote lazima uambatane na wasifu ulioandikwa kwa nafsi ya tatu na usiozidi maneno 100.

6. Hakikisha umetuma uwasilishaji ambao haujawahi kuchapishwa, isipokuwa kazi za tafsiri ambapo matini chanzo huenda ilikuwa imechapishwa.  


This text was translated by Prof. Kimani Njogu, a linguist, cultural scholar, writer, mentor, global leader and communications consultant. He is the CEO of Twaweza Communications, a strategic communications firm and the founder chairman of Chama cha Kiswahili cha Taifa, a body dedicated to the promotion of Kiswahili in Kenya. His book, Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu, coauthored with Rocha Chimera, won the 2000 Noma Award for Publishing in Africa. Prof. Njogu has also written a widely used Kiswahili dictionary.

What's Your Reaction?
Excited
2
Happy
1
In Love
0
Not Sure
0
Silly
0
Scroll To Top